
Waaamuzi wa mchezo huo akiwemo mwamuzi wa kati Emmanuel Mwandemba, waamuzi wasaidizi Mohamed Mkono na Ferdinand Chacha pamoja na mwamuzi wa akiba Jonesia Rukyaa, wamekutana na timu zote mbili na kuelezana taratibu na kanuni za mechi yenyewe ya fainali.
Katika mchezo wa nusu fainali kati ya Singida United na JKT Tanzania uliopigwa kwenye uwanja wa Namfua Singida, ulitokea utata juu ya kanuni ya mchezo ambapo timu ya JKT Tanzania walidai kuambiwa mchezo ungeishia dakika 90 na kwenda kwenye penati lakini Singida walidai wameambiwa mchezo unaenda dakika 120.
Mkutano wa jana pia ulihudhuriwa na mtathmini wa waamuzi Charles Mchau na Kamishna wa mchezo huo Mulamu Ng’ambi. Mchezo huo wa leo unatarajia kutoa mwakilishi wa nchi kwenye michuano ya Kombe la shirikisho Afrika.