Ijumaa , 22nd Jun , 2018

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amewataka wafuasi wake wanamfuatilia kwenye mitandao yake ya kijamii kumvumilia katika kipindi hichi cha kombe la dunia kwa kuonyesha mapenzi yake kwa mchezaji Cristiano Ronaldo kutoka timu ya Ureno.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara.

Manara ameamua kumwaga povu hilo baada ya kuonyesha mapenzi yake kwa Ronaldo ambaye ameonyesha kung'aa sana katika kombe hili la dunia huku mpinzani Lionel Messi akionekana kujikongoja kutokana na Timu yake kuendelea kufanya vibaya tangu kuanza kwa mashindano hayo.

"Guys kuna kitu naomba mkielewa hususani wale wasioelewa maana ya ushabiki, duniani kote kuna aina mbili ya mashabiki kwa hawa watu wawili na mimi ni team Ronaldo..na raha ya ushabiki ni kuzodoana..sasa Team Messi mmepanic kama mmefumaniwa jamani!" Manara

"Najua Messi ni mchezaji bora kama Ronaldo..but msilazimishe sote tupende mtakacho hii ndio raha ya ushabiki kama ilivyo Simba na Yanga".

Kwa  kusisitiza Manara amesema "Tuvumiliane na msijaribu kunipangia cha kushabikia na kupost..hii si acc ya Simba wala ya mtu yoyote ni yangu binafsi..sichangiwi na mtu bando".