
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema.
Lema amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ambapo amedai kuwa tatizo kubwa linalolikabili taifa kwa sasa ni kuwa wananchi wanadhani kuwa haki na demokrasia inatafutwa na wapinzani pekee.
“Watu wanafikiri masuala ya haki, usawa na utawala wa sheria ni wajibu wa CHADEMA hawa wana hitaji maombi na dua,jambo lolote linalohusu haki na demokrasia ni wajibu wa kila Mwananchi.Tatizo kubwa linalokabili Nchi kwa sasa ni kuwa na aina hii ya fikra hata kwa wanaoitwa wasomi”, ameandika Lema.
Kauli ya Lema imekuja ikiwa ni siku moja toka Menyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe kufunguka kuwa kudai kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa kesi inayowakabili.