
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola.
Kangi ametoa maamuzi hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo hicho, ambapo alionya wananchi ambao wamekuwa wakiwatumia askari polisi kuwaadhibu raia wengine.
“Nimewataka askari polisi warekebishe kasoro, leo mfanye operesheni maalum, ili ambao makosa yao yanadhaminika muwaachlie. Nitoe wito kwa wananchi, mutoe taarifa za kihalifu kituoni, ila pia niwaombe wananchi wasiwatumie polisi ili raia wenzao wakae mahabusu.”
“Mimi ni Mkurya wa Kijita leo hakuna kulala, ukae na watu wako mpitie mafaili yote ili muone watu gani ambao hawastahili kukaa kituoni,” amesema Kangi Lugola."
“Kazi yenu nyinyi watanzania ni kufurahi kwenye nchi hii ya Magufuli usipofurahi wewe ndugu mtanzania labda una matatizo.”
Hivi karibuni Waziri Kangi Lugola alikuwa visiwani Zanzibar ambapo alikutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.