
Wachezaji Gadiel Michael kushoto na Ibrahim Ajibu kulia.
Akiongea na www.eatv.tv kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Gadiel hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachocheza na Kagera Sugar kesho kwasababu imelazimika arejeshwe Dar es salaam kwaajili ya matibabu.
''Timu imefika salama hapa Kagera na tumefanya mazoezi kwa wachezaji waliopo kwenye timu isipokuwa Gadiel Michael ambaye ameumia nyama za paja hivyo imebidi arudi Dar es salaam kupata matibabu'', amesema
Zahera.
Kwa upande mwingine Zahera amesema programu yake ya mazoezi kuelekea mchezo wa Kagera Sugar inaendelea kwa wachezaji ambao hawakucheza mechi dhidi ya Mwadui kufanya mazoezi kwa saa 1:30.
Kwa wale ambao walicheza mchezo dhidi ya Mwadui FC, watafanya mazoezi mepesi. Yanga watakuwa wageni wa Kagera Sugar kesho Jumapili mchezo ambao utapigwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Kaitaba.