Jumatatu , 1st Apr , 2019

Mzoga wa nyangumi mjamzito ambao ulisombwa na maji hadi katika fukwe ya Sardinia nchini Italia, umekutwa na kilo 22 za plastiki tumboni pamoja na kichanga kilichokufa.

Nyangumi

Kwa mujibu wa Rais wa kundi moja la utunzaji mazingira la SeaMe nchini Italia, Luca Bittau, ameiambia CNN kuwa miongoni mwa vitu vilivyokutwa katika tumbo la nyangumi huyo ni mifuko ya uchafu, nyavu za kuvulia samaki, mabomba na mifuko ya sabuni za maji za kufulia nguo.

Nyangumi huyo mwenye urefu wa mita 8 na futi 26, alisombwa kutoka baharini hadi katika fukwe ya Sardinia, ambapo amesema kuwa chanzo cha kifo chake kitajulikana baada ya uchunguzi wa wataalamu wa wanyama nchini humo.

Naye Waziri wa mazingira wa Italia, Sergio Costa amesema kuwa serikali inalichukulia tatizo hilo kama changamoto kubwa katika utunzaji wa mazingira, akisisitiza kuwa nchi yake itakuwa ya kwanza kutekeleza sheria iliyopitishwa na bunge la Ulaya la kupiga marufuku kusambaa kwa vifungashio vya plastiki ili kulinda tishio la uhai wa viumbe wa majini.

Tukio lingine linalomhusu nyangumi

 

Licha ya tukio hilo, mwezi uliopita, nyangumi mwingine mdogo alikutwa amekufa nchini Ufilipino, akiwa na kilo 40 za plastiki tumboni.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.