
Kocha Patrick Aussems na wachezaji wa Simba
Simba ambao wametwaa mara 6 miaka ya 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002, imesema ratiba ya michuano hiyo inaingiliana na ratiba yao ya maandalizi ya msimu ujao wa 2019/20.
Simba ambao pia ni mabingwa wa kwanza wa kombe hilo lilipoanzishwa mwaka 1974, wamewataarifu mashabiki na wanachama wao kuwa hawatashiriki.
Taarifa kwa umma. #NguvuMoja pic.twitter.com/zLHUIKvGcn
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) June 7, 2019
Watani wa jadi wa Simba, timu ya Yanga ya Tanzania, imetwaa kombe hilo mara 5 katika miaka ya 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.