Jumatano , 3rd Jul , 2019

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha amefafanua sababu yeye ni kutumia salamu za Chama Cha Mapinduzi huku yeye akiwa Afisa wa Polisi ambaye hatakiwi kujihusisha na masuala ya siasa, huku akieleza hata salaam aliyoitumia haina uhusiano na chama hicho bali ni salamu yake binafsi.

Kamanda Shana amesema alialikwa kwenye kikao hicho kama Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha, ili kutoa taarifa kuhusiana na hali ya usalama huku sintofahamu kubwa ikijitokeza alipotumia kauli za Chama Cha Mapinduzi kwa kuwataka wajumbe wa mkutano huo kuitikia kauli ya kuwa 'CCM haina kulialia' kwa kuwa vyombo vya dola ni vyao.

Kamanda Shana amesema kuwa "ule ulikuwa ni mkutano wa ndani na mimi nilialikwa na Mkuu wa Mkoa kama sehemu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa katika kipengele cha ulinzi na usalama."

"Kama wanalalamika mimi nimetumia salamu ya CCM, kaangalie Katiba ya CCM kama kuna aina hiyo ya salamu, ule ni msemo wangu, mwisho nilisema chama tawala hakina sababu ya kulialia, je ni sawa mtawala kulialia." amesema Kamanda Shana

"Kama watasema nimerudia niliyoyafanya Butiama kwenye kumbukizi ya Mwalimu Nyerere, sasa kule walitaka niseme chama kife, nilisema Mwalimu amekufa chama chake kisife, sasa niambie walitaka niseme chama kife wakati nipo kwenye kumbukumbu ya mwalimu Nyerere." ameongeza Shana