Mo Dewji
Taarifa hizo zilianza kusambaa usiku wa jana katika mitandao ya kijamii, lakini mwenyewe amejitokeza na kuweka bayana kinachoendelea.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji amesema, "watu wenye nia mbaya. Kazi yao sio kujenga, ni kuvunja tu. Kaa nao mbali. Narudia kaa nao mbali sana!".
Hii leo, Julai 5, katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Mo Dewji ametoa ujumbe mwingine unaoelezea kile kinachoendelea hivi sasa ndani ya klabu hiyo.
Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi - mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao. pic.twitter.com/eDTkHWgAgl
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 5, 2019