
Bashe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV/Radio Digital juu ya kuteuliwa kwake kuwa na Rais Magufuli, taarifa ambayo ilitolewa asubuhi ya leo, kupitia kwa kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.
Bashe amesema, “mimi niseme tu kwanza nimshukuru Rais kwa imani yake kwangu ambayo amenipa, kwa hiyo jukumu langu nimepewa kwenda kumsaidia Waziri Japhet Hasunga, kwenda kuhakikisha tunafikia malengo na matamanio ya Watanzania”.
Bashe amesema, “hii ndio sekta iliyoajiri Watanzania wengi, inaendesha uchumi wa nchini inachangia 28 ya GDP na asilimia 70 ya ajira lakini ina changamoto nyingi, nina amini katika ushirikiano tutafanikiwa”
Fuatilia mahojiano kamili hapo chini.