Jumanne , 24th Sep , 2019

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya 'MMB', Madee amepiga stori na EATV & EA Radio Digital na kunyoosha maelezo kuhusu Jux kwamba ndiye msanii bora wa RnB na kuvunjika kwa mahusiano yake na Vanessa Mdee.

Jux na Vanessa Mdee

 Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Madee alimtaja Jux kuwa ndiye msanii wake bora wa RnB nchini Tanzania, jambo ambapo lilipelekea kuzuka kwa maswali kuwa ni sababu gani zimepelekea kutoa heshima hiyo.
 
Akijibu suala hilo Madee amesema, “mimi hayo ni mawazo yangu sidhani kama kuna ruhusa ya mtu kunipinga, sitaki kumlazimisha mtu mwingine na yeye ampende Jux au ningeendelea kubaki nalo moyoni mpaka lini au mlitaka hadi siku Jux anakufa ndiyo niseme alikuwa mwanamziki wangu pendwa itakuwa sio. Kitu kizuri ni kheri kusema mapema wakati yupo hai mwenyewe anaona”.

Madee ameendelea kusema kuwa kitu anachovutiwa na Jux ni jinsi anavyoimba, muonekano wake nje ya muziki na kuwa kwenye 'game' kwa muda mrefu bila kutetereka.

Akizungumzia kuhusu kuvunjika kwa mahusiano ya Jux na Vanessa Mdee amesema, “wanaachana watu waliopo kwenye ndoa sembuse mtu na mpenzi wake, nimeona ni kawaida tu halafu ukizangatia bado vijana, wana marafiki wengi, ni watu maarufu kwahiyo ile mikiki ya nje kuhusu mapenzi bado itawachanganya tu”.