Mo Dewji akiwa katika ukaguzi wa uwanja
Klabu hiyo iko katika mkakati wa ujenzi wa kituo chake ambacho kitakuwa na viwanja vya mazoezi, hosteli za wachezaji pamoja na 'gym', ambapo katika hatua ya kwanza ikianza na ujenzi wa viwanja viwili.
Akizungumza alipotembelea viwanja hivyo, Mo amesema kuwa hivi karibuni viwanja hivyo vitakamilika pamoja na vyumba vyake vya kubadilisha nguo.
Leo asubuhi nilitembelea viwanja viwili vya mazoezi vya Simba vilivyopo Bunju kuangalia maendeleo. Nina habari njema: kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba, uwanja wa nyasi asilia na nyasi bandia pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo vitakuwa vimekamilika Insha’Allah! pic.twitter.com/ZifmGfLmUJ
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) September 28, 2019
Klabu ya Simba ipo kanda ya ziwa ikiendelea na mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo katika mchezo wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, mchezo uliopigwa Septemba 26, 2019 katika uwanja wa Kaitaba.




