Jumapili , 10th Nov , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machari, ameikaribisha klabu ya Yanga Wilayani kwake ambayo imeenda huko baada ya kushinda mchezo wake wa Ligi kuu dhidi ya Ndanda FC Ijumaa iliyopita.

Wachezaji wa Yanga na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu

“Tumefurahi sana kwa ujio wenu, mnadhihirisha kwa vitendo kuwa hii ni timu ya Wananchi, Karibuni sana Wilayani Nanyumbu.” Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Moses Machari.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amekiri kuwa yeye ni shabiki Mkubwa wa Yanga tangu akiwa mdogo ila sio mwanachama lakini kama wanataka kumpa kadi wanaweza kufanya hivyo.

Pia amewasifu Yanga na kuweka wazi kuwa wao kama Wilaya ya Nanyumbu ni sehemu ya Tanzania na wanapenda wageni watembelee huko hivyo ujio wa Yanga wameupokea kwa furaha.