
Mwenyekiti CHADEMA Taifa Freeman Mbowe
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, amesema mfumo utawasaidia kukusanya karibia Bilioni 5 kwa mwaka.
Mbowe amesema "Leo tunazindua mfumo wa Kidigitali tutahama kutoka Analog tutahamia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, tunahitaji kujenga chama kitakachojitegemea, kwa sababu Serikali inafikiri chama hichi kinategemea sana Ruzuku"
Aidha Mbiwe amesema kuwa "Hatutambui Uchaguzi wowote uliofanyika wa Serikali za Mitaa, kokote ambako wagombea walikuwepo watengeneze Serikali Vivuli kuangalia matatizo ya wananchi"
"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa niliwatafuta Wakuu wa Ulinzi na Usalama nikawaambia mnatuchokoza, halafu mtasema sisi tuna vurugu, inabidi wawaambie Mabosi wao, wakitimuliwa kazi njooni CHADEMA tutafanya wote kazi." - @freemanmbowetz - Mwenyekiti CHADEMA#MkutanoMkuuCHADEMA pic.twitter.com/kWRpHU6luU
— East Africa Radio (@earadiofm) December 18, 2019