Jumatano , 22nd Jan , 2020

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amekutana na Makamanda wa Polisi wa Mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa, kwa lengo la kuweka mikakati na mpango kazi wa pamoja katika kushughulikia matukio ya mauaji yanayojitokeza.

Akiwa mkoani Shinyanga IGP Sirro, amewaonya wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya imani za kishirikina, vinavyopelekea mauaji.

Aidha, IGP Sirro amemuagiza Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Nchini, CP Liberatus Sabas, na Makamanda wote wa Mikoa ya Shinyanga, Geita, Kagera,Mwanza na Simiyu, kufanya operesheni ya pamoja itakayosaidia kukomesha vitendo vya mauaji nchini.