
Kutokea upande wa kushoto ni Killy, Tommy Flavour na Cheed
Akiieleza EATV & EA Radio Digital, msanii huyo amesema yeye ndiyo amepitia kipindi kigumu kuliko wengine na suala la kuondoka kwao haihusiani na yeye, kwani kila mtu alipewa nafasi yake.
"Taarifa za kuondoka kwao zilinipata nikiwa nyumbani na niliziona mitandaoni wakiwazungumzia, sikuwa na ubaguzi na wote walikuwa washkaji zangu na Kings ilitoa nafasi kwa kila msanii, mimi sio sababu ya wao kutoka kwanza mimi ndiyo nilipitia kipindi kigumu zaidi, maana nimechelewa kutoa kazi na kuna mambo yalitokea kwahiyo kama ingekuwa wa kukasirika basi ningekuwa mimi" ameeleza Tommy Flavour.