Jumatano , 12th Aug , 2020

Mshambuliaji Bernard Morrison ameshinda kesi dhidi ya Klabu ya Yanga, na kuamuliwa kurejesha fedha alizopewa na Klabu hiyo jumla dola elfu ishirini na tano.

Winga Bernard Morrison akisaini mkataba wa kutitumikia Klabu ya Simba

Uamuzi huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Elias Mwanjala ambaye amesema amekuwa mchezaji huru kwa kuwa Mkataba baina yake na Yanga ulikua na utata na mapungufu .

Mkataba uliokuwepo wa miezi sita ulimalizika Julai 14, lakini mkataba wa pili ambao ni wa miaka miwili una mapungufu makubwa ambayo ni tarehe ya Mkataba.

Mwanjala amesema tarehe ya Mkataba unaonyesha alisaini Mkataba Machi 20 mwaka huu,lakini mkataba halisi unaonyesha Morrison alisaini Julai 15, mwaka huu, huku ukiwa na mapungufu ya sehemu ya kusaini pande zote mbili ambao ulikatwa ikiashiria hakukua na maridhiano.

Katika hatua nyingine, Mwanjala amesema licha ya kumpa uhuru Morrison, kamati itampelea kwenye kamati ya maadili kwa kusaini mkataba na Klabu nyingine wakati kesi yake ilikuwa kwenye kamati hivyo alidharau kikao.