Jumatano , 26th Aug , 2020

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla ametoa somo kuhusiana na suala zima la mahusiano kwa kusema kama ulimpenda mtu na akakusaliti au kukuumiza basi unatakiwa kumshukuru Mungu kwa sababu hujui kipi kimekuondosha kwenye mikono yake.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla

Dkt Hamisi Kigwangalla ametoa somo hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo aliipa hashtag ya #Mapenzi_101 huku akitoa mtazamo wake juu ya kufanya endapo ukisalitiwa kwenye mahusiano.

"Ukiondoka kwenye mahusiano ya kimapenzi kamwe usijute kwa mema uliyomfanyia mwenzako enzi ukiwa naye, maana ulitimiza wajibu wako sema kwa mtu asiyestahili, Songa mbele kwa furaha, huko kuna furaha yako

"Ukiachwa na mtu uliyempenda kwa dhati ya moyo wako wala usijisikie vibaya, ukajihisi wewe ni mbaya, haufai, una mkosi au umekosea la hasha amini kuwa yeye ndiye amekupoteza wewe na hajui thamani ya kupendwa, alikuja kwako kwa malengo, Mungu anajua zaidi" ameongeza

Aidha Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amemaliza kwa kuandika "Kama ulimpenda mtu kwa dhati na akaamua kukupiga chini, ama kuku-mistreat mshukuru Mungu, songa mbele katafute furaha huko, hujui kwa nini Mungu amekuondoa kwenye mikono yake,  Hakika anayekupenda hawezi kuku-mistreat wala kukuacha uteseke"