
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni SACP Edward Bukombe.
limewakamata watu thelathini kwa makosa ya wizi.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni SACP Edward Bukombe wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya usamala ilivyo katika mkoa wake ambapo pia ameonyesha mali za wizi zilizokamatwa na jeshi hilo zikiwemo pikipiki tano gari moja na vifaa mbalimbali vya ndani.
"Niwatake watanzania hasa wale waliojipanga kufanya vurugu Jeshi la Polisi limejipanga na hawatoweza kufanya vurugu" amesema SACP Edward Bukombe, Kamanda wa Polisi Kinondoni.
Aidha, amewataka wakazi wa Kinondoni na wote wanaoingia kufuata taratibu za kisheria ili kuepuka majanga huku akiwatahadharisha pia wanaotumia mitandao kufanya uhalifu wa wizi wa pesa na kutuma picha za utupu.
Amesema kwa sasa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni umetulia licha ya kuwapo kesi za uporaji wa kutumia Bodaboda maarufu kama ‘vishandu’ huku akiwaasa wakazi wa Kinondoni kuwaripoti watu wanaohisi kupanga njama za kihalifu.