Ijumaa , 23rd Oct , 2020

Manispaa ya Temeke imeandaa zoezi la upimaji macho bure na wale watakaobainika kuwa na matatizo watapatiwa ushauri na madaktari na wengine ambao wanaweza kupatiwa matibabu watatibiwa papo kwa hapo.

Pichani ni zoezi la upimaji macho

Kaimu mratibu wa macho manispaa ya Temeke, Daniel Hebron Ringo, amesema zoezi hilo linalenga kusogeza huduma kwa wananchi ili wale ambao wamezikosa waweze kuzipata

“Kuna idadi kubwa ya wananchi wa Temeke ambao wana matatizo ya kiafya ikiwemo macho kwa hiyo kwa kulifanya zoezi hili tunawasaidia waweze kupata matibabu” amesema Ringo

Aidha Mratibu huyo ameogeza kuwa licha ya kwamba zoezi hilo ni la siku moja lakini litakuwa ni endelevu katika manispaa hiyo kadri ya watakavyokuwa wanajiandaa kwa ajili ya kumaliza tatizo la macho katika wilaya hiyo.