
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu
Kauli hiyo imetolewa na Dkt.Jingu katika mkutano wake na Jukwaa la Wahariri nchini TEF uliofika Ofisini kwake kutambulisha maandalizi ya tuzo za Waandishi wa Habari kuhusu watoto ambapo amewataka waandishi kutafiti na kuainisha masuala yahusuyo watoto ili kujenga Jamii yenye mtazamo chanya.
“Wakati mwingine mwandishi anaibua tatizo halafu anawaacha hewani kumbe na yeye ni mdau anatakiwa kutoa mchango wa kutafuta jawabu, tukiwa na waandishi wenye majawabu watatusaidia sana” amesema Dkt. Jingu.
Aidha Dkt.Jingu amesema kuwa ni muhimu kwa waandishi wa habari kuandika habari zinazoijenga Jamii na kutafuta changamoto zinazowahusu watoto badala ya kujikita katika ukosoaji pekee huku akidai kuwa waandishi ni muhimu kuleta mabadiliko.
Hata hivyo, Dkt. Jingu amewahimiza waandishi wa habari katika maeneo mbalimbali nchini kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Haki ya Mtoto, itakayofanyika tarehe 20 Desemba 2020, ikiwa na kauli mbiu ‘Dunia salama kwa kila Mtoto inawezekana; Chukua hatua’.