Jumanne , 29th Dec , 2020

Mchezo wa mpira wa miguu unaongoza kuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi, ukilinganisha na michezo mingine, na Tanzania inajumla ya wanamichezo 54 wanaocheza michezo ya kulipwa nje ya nchi, hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Innocent Bashungwa.

Mchezo wa mpira wa miguu ndio mchezo unaoongoza kuwa na wachezaji wengi 28, miongoni mwa wachezaji wanaocheza michezo ya kulipwa nje ya nchi.

Waziri Bashungwa alitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumza na wachezaji wa zamani wa timu za taifa za michezo mbalimbali hapa nchini, ikiwa ni katika harakati za kukusanya maoni ya wachezaji hao wa zamani ili kuangalia ni kwa namna gani michezo hapa nchini inaweza kurejesha heshima yake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Katika kuonyesha jitihada za serikali kwenye kusaidia kuinua michezo nchini, Waziri Bashungwa alisema tangu yalipofanyika mabadiliko ya sheria ya Baraza namba 12 ya mwaka 1967, ili kutambua michezo ya kulipwa hapa nchini, baada ya mabadilko hayo ya sheria hivi sasa Tanznaia ina jumla ya wachezaji 2,280 ambao wanacheza michezo ya kulipwa hapa nchini na nje ya nchi kutokana na mabadiliko ya hiyo sheria ya mwaka 67.

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Innocent Bashungwa

 

Mh. Waziri akaweka bayana idadi ya wachezaji wanaocheza michezo ya kulipwa nje ya nchi.

“Lakini ukiangalia idadi ya wachezaji walioajiriwa nje ya nchini mpaka hivi sasa wapo 54, au wameshaongezeka kwa takwimu za leo, kwenye soka tunavijana ambao wapo nje ya nchi 28, wanacheza soka la kulipwa, kikapu yani (basketball) wapo 16, upande wa mpira wa wavu (netball) wapo kuna vijana 4 ukienda wawili hapa waili pale jumla 54”, amesema Bashungwa.

Hizi ni takwimu ambazo zilitolewa mbela ya wachezaji wa zamani wa timu za taifa za michezo mbalimbali hapa nchini na Waziri Bashungwa ikiwa ni kuonyesha jitihada za Serikali kwenye kutengeneza usatawi bora wa michezo nchini.