Jumatatu , 1st Feb , 2021

Mwanamuziki mkongwe na Malkia wa muziki hapa nchini Tanzania, Lady Jaydee, ama Komando Jide, amesema kuwa muziki wa sasa haudumu na unawahi kupotea kwenye masikio ya watu kwa sababu upo kama 'bubble gum' hivyo utamu ukiisha lazima uiteme.

Mwanamuziki Lady Jaydee

Kauli hiyo ameitoa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television (EATV), kinachoruka kila siku za Ijumaa kuanzia saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, baada ya kuulizwa kwanini muziki wa zamani unaishi mpaka sasa na muziki unaofanywa na wasanii wa siku hizi unawahi zaidi kupotea.

"Wasanii wa siku hizi wanafanya 'bubble gum music' unakuwa ni muziki wa muda mfupi tu ili uwalipe kwa hapo hapo lakini 'in a long run' hakuna muziki", amesema Lady Jaydee

Tazama video hapa