Jumatatu , 15th Mar , 2021

Timu ya Philadelphia 76ers ya ligi kuu ya kikapu  mchini Marekani, leo tarehe 15 Machi 2021 imethibitisha kuwa mchezaji wake nyota, Joel Embiid atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 2 hadi 3 baada ya vipimo vya MRI kuonesha amevunjika mfupo mdogo kwenye goti lake la kushoto.

Mchezaji nyoTa wa timyu ya Philadelphia 76ers, Joel Embiid baada y akupata maumivu ya goti.

Embiid alipata majeraha hayo wakati timu yake ilipocheza na Washington Wizard Ijumaa iliyopita na  kugongana na mlinzi wa timu hiyo jambo lililopelekea adondoke vibaya na kuumia kwenye goti lake.

Embiid aliondoka uwanjani robo ya tatu akiwa tayari amepata alama 23, ribaundi 7, kutengeneza mabao 3 na kuzuia mashambulizi 2 ya Washington Wizard.

Mashabiki wa Philadelphia 76ers watakuwa wenye simanzi kwani kuongoza kwao ligi upande wa Mashariki umechagizwa na uwezo mkubwa wa nyota huyo kikosini.

Kuumia kwa nyota huyo pia, kumeweka hatiani uwezekano wake wa kushindania tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo 'MVP' kwa msimu huu kuwa ngumu kwani nyota wa mabingwa watetezi, Lebron James wa LA Lakers anazidi kuonesha kiwango bora zaidi.

NBA inatazmiwa kuendelea tena alfajiri ya kesho kwa michezo 8, huku ule wa kukata na shoka ni ule utakaowakutanisha Golden State Warriors ya Stephen Curry na Los Angeles Lakers ya Lebron James mchezo utakaochezwa saa11:30 alfajiri ya kuamkia kesho tarehe 16 Machi 2021.