Jumanne , 23rd Mar , 2021

Nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard ameshangazwa na kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate kwa kutomjumuisha mlinzi wa kulia wa Liverpool Trent Alexander Arnold kwenye kikosi cha wachezaji 26 watakao cheza michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022.

Trent Alexander Arnold

Trent hakujumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 26 kilichoitwa wiki iliyopita, ambacho kipo kambini kujiandaa na michezo mitatu ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia zitakazo fanyika mwaka 2022 Qatar, kikosi hicho cha Simba watatu kinakabiliwa na michezo dhidi ya San Marino, Albania na Poland.

Kocha wa England Southgate aliweka wazi sababu za kumacha mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 22 ni kutokana na kutokuwa kwenye kiwango bora kwa sasa, ukilinganisha na wachezaji wengine wanao chezaji nafasi hiyo ya mlizi wa kulia ambao ni Kyle Walker, Kieran Trippier na Reece James.

Gerrad aliichezea Liverpool kwa miaka 17 na sasa ni kocha wa Rangers ya Scoutland, anaamini Trent ndio mliznzi bora wa kulia kwenye ligi kuu England, na kwa kipindi hiki ambacho hayupo kwenye kiwango bora Kocha alipaswa kuwa karibu zaidi na mchezaji kuliko mtu yoyoyte hivyo ameshangazwa mchezaji huyo kutojumuhishwa kwenye kikosi.