
Msanii Anjella kushoto, kulia ni aliyekuwa mburudishaji wa FNL Ibiza Boy
"Kwa niaba ya Konde Music Wordwide tunatoa pole kwa EATV nzima kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, namfahamu Ibiza Boy kama mtoto wa mwenye nyumba yangu sehemu ambayo nilikuwa naishi na rafiki yangu"
"Alikuwa hakai pale alikuwa anakuja na kuondoka, akija kuangalia mazingira pale mimi nipo, tulikuwa tunakumbukana ila mazoea tulikuwa hatuna nilivyomkuta huku nilifurahi na nilishtuka pia, nikaamini kweli milima haikutani binaadam tunakutana" ameeleza Anjella.
Ibiza Boy alifariki dunia siku ya Aprili 18 kwa ajali ya gari, na siku ya Aprili 23 amezikwa katika makaburi ya Kisota Kigamboni.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.