Jumatano , 28th Apr , 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa msisitizo Juu ya suala la kuchukuwa hatua kuhusu Athari za kuweza kukabiliana na Majanga yanayohusiana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango akifanya mazungumzo na Bibi Mary Ngelela Maganga Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ofisini kwake Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango amesema kubwa ni kuwaelimisha Wananchi kuhusu kujuwa Athari zinazotokana na uharibifu wa Mazingira pamoja na kuchukuwa hatuwa Madhubuti ya kuzuwia uharibifu wa Mazingira kwa kupanda miti isiyoweza kuleta Mazara.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo April 27,2021 alipokutana na kufanya mazungumzo na Bibi Mary Ngelela Maganga Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ofisini kwake Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Kuhusu suala la kuimarisha Muungano Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdir Mpango amesema kuna haja kubwa ya kuwekeza kwenye Elimu katika Sekta mbalimbali ikiwemo Mashuleni na Viongozi wa Dini ili kujuwa Changamoto zitakazojitokeza na kuweza kutatuliwa kwa kukaa pamoja baina ya pande zote mbili za Muungano.

Tazama Video hapo chini