
Raheem Sterling
Micah Richards ameyasema hayo kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya usiku wa leo ambapo Manchester City watakua ugenini kuwania nafasi ya kuzufu hatua ya fainali dhidi ya PSG.
Wakati anazungumzia juu ya kupanda na kushuka kwa kiwango cha Sterling Richards amesema,
“Kuna wakati anaweza kupata msongo wa mawazo akiwa chini ya kiwango, lakini ameonyesha jinsi anavyo stahimili na kutuliza kichwa chake na baadaye anarudi kwenye kiwango chake kizuri na hiki ndio kilitokea hata kwenye mchezo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Tottenham.”
Raheem Sterling alikumbana na ukosoaji mkubwa sana kutoka kwa wachambuzi wa soka baada ya kuonyesha kiwango cha chini kwenye mchezo wa fainali ya Carabao CUP dhidi ya Tottenham, mchezo ambao ulichezwa Jumapili ya Mei 25, 2021 katika dimba la Wembley na Manchester City iliibuka na ushindi wa bao 1-0.