
Mashabiki wa Mbeya City
Mbeya City waliingia kwenye mchezo wa jioni ya leo wakiwa nafasi ya 17 na alama 27, lakini baada ya ushindi huu mkubwa walioupata wamepanda mpaka nafasi ya 13 kwenye msimamo na wamefikisha alama 30, na ushindi wa leo unakuwa ni ushindi wa tatu mfululizo baada ya kushinda michezo miwili iliyopita dhidi ya Polisi Tanzania na Namungo FC.
Mabao ya wanakoma kumwanya yamefungwa na Kibu Denis Dakika ya 19, David Mwasa dakika ya 45, Richardson Ngodya dakika ya 49 Juma Luzio amefunga mara mbili dakika ya 68 na 88 na bao la 6 lilifungwa na Pastory Athanas. Huu unakuwa ushindi mkubwa zaidi kwa Mbeya City msimu huu kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Kwa kipigo cha hii leo JKT Tanzania wameporomoka kutoka nafasi kya 15 hadi ya 17 kwenye msimamo wakisalia na alama zao 27. Na huu ni mchezo wa pili mfululizo wanafungwa na katika michezo 6 ya mwisho wamefungwa michezo 5 na wameshinda mchezo mmoja tu.