Mtangazaji Bhoke Egina
Akizungumzia hilo kupitia show ya DADAZ ya East Africa TV kwenye 'Lifestyle Tuesday' wakati wanapiga stori juu ya utaratibu wa kununua nguo za ndani mara kwa mara Bhoke Egina amesema
"Nguo za juu huwa sio mnunuaji navaa moja hata kwa mwaka mzima labda ipate hitilafu, mwanamke unaweza ukawa na brazia nyingi lakini kuna ile moja ambayo ukivaa unakuwa 'comfortable' na unayoipenda, unavaa mpaka iseme basi au kuomba poo, za chini sina matumizi nazo kwa hiyo sinunui"
Aidha Najma Paul amesema "Siwezi kutembea bila kuvaa nguo ya juu au ya chini, za juu nikinunuaga huwa sipendi vichuma vinaniumiza sana ila ninazo nyingi, za chini napendelea taiti"
Na kwa upande wa Mwanne Binti Othman kuhusu nguo za ndani amesema huwa ananunua 'Dozen' mbili kwa mwaka huzivaa na zikiacha kuchoka anazitupa na kununua zingine.
Zaidi tazama hapa kwenye video.