
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.
Maneno ya Pep yanakuja baada ya ligi kuu ya England maarufu 'EPL' kutangaza visa kumi na moja vya covid-19 kwa wachezaji na makocha mbalimbali wakiwemo Willian, Alexander Lacazette, Pierre Emerick Aubameyang wa Arsenal na Christian Pulisic wa Chelsea.
Guardiola amesema, “Nafikiri njia sahihi ni kuwaelezea wachezaji faida na hasara ya kupata au kutokupata chanjo ya Covid-19 kwa ajili yao, kwa ajili ya familia zao na faida kwa watu wote wanaofanyakazi hapa na huko mtaani. Na baada ya baada ya hapo, kila mtu atafanya maamuzi”.
“Lakini, pale wanasayansi wote, madaktari wote, wataalam wote wa dawa wakisema suluhu pekee ya kuutokomeza au kusaidia kusonga mbele baada ya miaka hii miwili ya ugonjwa huu ni kupata chanjo, nafikiri wachezaji inabidi wafikirie kupata chanjo”.
Pep anaungana na baadhi ya makocha wengine wanaopendekeza wachezaji wapataiwe chanjo ili kujikinga na ugonjwa huyo ambao ni, kocha wa Arsenal , Mikel Arteta, Nuno Espirito Santo kocha wa Tottenham Hotspurs, Steve Bruce kocha wa Newcastle United na kocha wa Brighton & Hove Albion, Graham Potter.
Manchester City inayoshika nafasi ya 12 baada ya kufungwa 1-0 na Spurs itashuka dimbani saa 11:00 jioni ya leo kucheza dhidi ya Norwich kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa EPL utakaochezwa kwenye dimba la Etihad, nyumbani kwa matajiri hao wa jiji la Manchester huku Norwich ikishika nafasi ya pili kutoka mwisho baada ya kufungwa mchezo wake wa kwanza.