
Kala Jeremiah kushoto, kulia ni Nay wa Mitego
Kala ametoa kauli hiyo wakati akitoa comment yake kuhusu wimbo mpya wa rais wa kitaa ya Nay wa Mitego ambapo amesema kuwa.
"Nay wa mitego muziki wake ndio huo anapendaga kuja na ukakasi mwingi kwa sababu ndio uliomtoa, nia aina yake ya sanaa watu wanamjua na wamemzoea"
Aidha ameongeza kusema watu wawatii wenye mamlaka na ameshauri kwamba hata unapomchana mtu mwenye mamlaka unatakiwa utumie lugha iliyokaa kimamlaka ili aweze kukusikiliza na asione kama unamshambulia.