
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho hayo Dkt Noel Lwoga, wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa maboresho ya kituo cha Makumbusho ya Azimio la Arusha na Makumbusho ya Elimu Viumbe inayotekelezwa chini ya mpango wa miradi ya ustawi wa nchi na mapambano dhidi ya UVIKO-19.
"Makumbusho ya Taifa ni moja ya taasisi iliyoathirika sana kimapato kutokana na ugonjwa wa Corona ambapo kumekuwa na upungufu mkubwa wa watalii wa ndani na nje ya nchi na kuathiri mapato hivyo tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia viongozi wa Wizara yetu ya Maliasili na Utalii kwa kuipatia fedha Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kutekeleza miradi katika vituo sita na maeneo ya malikale sita" amesema Dkt Lwoga