Alhamisi , 28th Apr , 2022

Ikiwa imesalia siku mbili kuelekea kwa mchezo wa Kariakoo Derby baina ya Yanga dhidi ya Simba ,Afisa habari wa Yanga Hajji Manara amesema wataingia kwenye mchezo huo wakitumia mfumo wa jihadi(kupambana) ili kupata ushindi kwenye mchezo huo.

(Afisa habari wa Yanga Haji Manara)

“tunakwenda tukiwa tunawaheshimu ila kwenye nafsi zetu wao na sisi tunajuana ,ukiona kifaru anakuja uku kainama ujue kuna jambo,kitu kimoja wajiandae nacho tutawapress na uzuri wake tunakundi kubwa la vijana na wenye kasi ,kocha wao ajindae kutuzuia jumamosi na tutacheza kwa jihadi mana ndio asili yetu” amesema Manara

Katika upande mwingine,Mwenyekiti wa timu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msolla amemkabidhi kadi ya uwanachama wa klabu ya Yanga ,afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara kwenye makao makuu ya klabu ya hiyo Jangwani.

kamati ya utendaji iliridhia kwa pamoja kumchukua hajji , na mengi yalisemwa ujio wake lakini tunashukuru wengi walifurahia ujio wake na leo namkabidhi kadi yake ya uwanachama na nikutake wewe na wenzako wa idara ya habari tusaidieni kupata wanachama million 1 tufike mpaka million 2 “amesema Dkt Msolla

Yanga na Simba zitakutana kwenye dimba la Benjamin Mkapa mnamo April 30 siku ya Jumamosi majira ya saa kumi na moja kamili jioni  kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara huku mwamuzi wa mchezo huo akiwa ni Ramadhani Kayoko kutoka Dar es Salaam.