Ijumaa , 29th Apr , 2022

Timu ya taifa ya Tanzania ya wasichana umri chini ya miaka 17 Serengeti girls jumapili hii tarehe 1 mwezi wa tano 2022 wanatarajia kushuka dimbani katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu wa wasichana umri chini ya miak 17 ya burundi.

(Serengeti Girls wakiwa mazoezini Zanzibar)

Mchezo huo wa mkondo wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia kwa wasichana umri chini ya miaka 17 itakayofanyika nchini India baadae mwaka huu, utapigwa katika uwanja wa Amani visiwani zanzibar majira ya sa 10 jioni jumapili hii .

Serengeti girls imeweka kamabi visiwani Zanzibar na inaendelea na mazoezi katika uwanja huo wa Amani visiwani huo kujianda na mchezo huo wa kuwania kufuzu kombe la dunia chini ya kocha mkuu Bakari Shime. Serengeti girls inaingia kwenye mchezo huo wa jumapili wakiwa mbele kwa faida ya magoli 4 kwa sifuri walioshinda katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika nchini Burundi wiki mbili zilizopita.