Ijumaa , 6th Mei , 2022

Siku ya jumatatu wiki hii, ndege ya Virgin Atlantic iliyokuwa inatoka mji wa London, Uingereza kuelekea New York, Marekani ilighairisha safari yake na kurudi mji wa London baada ya kugundua moja wa marubani katika ndege hiyo alikuwa hajamaliza mtihani wake wa mwisho wa kuruka na ndege.

Ndege hiyo ilikuwa imejaa abiria na walikuwa wameshatumia dakika 40 tangu waondoke katika uwanja wa ndege wa Heathrow.

Rubani wa ndege hiyo aligundua msaidizi wake alikuwa hajamaliza mafunzo ya mwisho ya kuruka na ndege ya shirika la Virgin Atlantic hivyo akaghairisha safari ili kumbadilisha msaidizi wake.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uingereza ilitoa taarifa rubani huyo msaidizi amekidhi vigezo vyote vya kuruka na ndege na alipatiwa leseni, mafunzo ambayo hajafuzu labda ya kwao Virgin Atlantic.