Jumamosi , 11th Jun , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kujipanga ili kuweza kuhudumia mradi wa uchakataji wa gesi asilia na kupelekea mapato kubaki nchini na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wetu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais samia ametoa wito huo katika hafla ya zoezi la utiaji saini wa makubaliano ya awali ya mkataba wa kuchakata gesi asilia, baina ya serikali na makampuni yaliyongundua gesi kwenye vitalu namba 1,4, 2 na katika kina cha bahari ya hindi Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Aidha Rais Samia ameagiza kuimarishwa kwa taasisi zetu za udhibiti wa kodi, sheria pamoja na ulinzi, ili kusaidia katika ulinzi na uratibu wa mradi huo.

"Mradi wa LNG ni Biashara na uwekezaji mkubwa unahitaji tuimarishe taasisi zetu za udhibiti wa kodi, sheria pamoja na ulinzi, mradi huu ni mkubwa lazima ulindwe na walindaji wa mradi huu ni sisi sio wawekezaji" – Amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini January Makamba amesema mradi wa LNG utaenda sambamba na uwekaji wa miundombinu katika maeneo husika ya mradi huo, hivyo utawanufaisha moja kwa moja watanzania huku ajira elfu kumi zikitarajiwa wakati wa ujenzi wa mradi huo.