Jumatatu , 13th Jun , 2022

Klabu ya Yanga imemuongezea kandarasi ya miaka miwili kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Farid Mussa Malik kuendelea kuwatumikia wababe hao wa Jangwani hadi mwaka 2024 huku wakiwa na mpango wa kusajili nyota 4 tu wa kimataifa.

(Mgombea wa Urais wa Yanga SC, Eng.Hersi Said akiwa na Farid Mussa)

"Kwa usajili wa ndani hatuna presha ya watu na tunaleta hawa kwa ajili kutetea ubingwa wetu na ushiriki wetu wa michuano ya kimataifa na tutasajili wachezaji 4 au 5 wa kimataifa tu huku wachezaji hao wamecheza katika ligi kuu ya Afrika Kusini, Ivory Coast, Angola pamoja na mmoja kutoka Afrika Mashariki na hatujataja majina yao kwa sababu wengine wana mikataba na vilabu vyao" amesema Manara.

Miongoni mwa wachezaji wanaodaiwa kukamilisha usajili wa kujiunga na Yanga SC kwa msimu ujao ni Stephane Aziz Ki na Lazarous Kambole.