
Worriors wanahitaji ushindi katika mchezo 1 kutangazwa mabingwa wa NBA msimu huu
Kwa matokeo haya Golden State wanaongoza kwa ushindi wa michezo 3-2 katika michezo 5 iliyochezwa kwenye mfululizo wa michezo 7 ya fainali. Na sasa Worriors wanahitaji ushindi katika mchezo 1 tu katika michezo miwili iliyobaki kuwa mabingwa wa NBA msimu huu wa 2021-22.
Katika mchezo huu nyota wa Golden state worriors Andrew Wiggins amefunga alama 26 rebound 13 na pasi za kufunga (Assist) 2, Stephen Curry amefunga alama 16 pasi za kufunga (Assist) 8 na rebound 3. Na klay Thompson kafunga alama 21 pasi za kufunga (Assist) na rebound 3.
Mchezaji nyota wa Boston Celtics Jason Tatum ndiye mchezaji aliyefunga alama nyingi kwenye mchezo huu amefunga alama 27, lakini pia amechukua rebound 10 na pasi za kufunga (assists) 4.