
Andy Murray
Bingwa huyo mara mbili wa Wimbledon alisema amekuwa ameweza kufanya mazoezi vizuri lakini kuna baadi ya mikimbio na mapigo hajaweza kupiga kufuatia jeraha hilo.
"Jeraha linapona lakini bado si kamilifu, na lengo langu ni kuanza michuano hiyo nikiwa na hali nzuri ya kimwili na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri." Alisema Murray
Murray mwenye umri wa miaka 35 alipata jeraha hilo kwenye fainali ya Stuttgart tarehe 12 Juni, 2022 na baadae akajiondoa kwenye shindano la Queen siku moja baadaye.
Muingereza huyo aliyeorodheshwa katika nafasi ya 51 ya viwango vya ubora duniani, amekuwa akifanya mazoezi kwenye uwanja wa nyasi kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo ya Grand Slam itakayoanza Jumatatu ijayo.
Ikumbukwe Murray alishinda taji hilo mwaka 2013 na 2016, anasema bado anakimbizan ana muda kujiweka vizuri japo ana mataumaini makubwa kwamba ataweza kushiriki michuano hiyo.