Alhamisi , 30th Jun , 2022

Vikao vya Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vimeahirishwa hadi Septemba 13, 2022, wabunge watakapokutana tena.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Akitoa hoja ya kuahirisha Bunge hilo hii leo Juni 30, 2022, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wabunge kwenda majimboni kwao kuwaeleza yale yote yaliyojiri katika vikao vyake wananchi wanaowawakilisha.