Alhamisi , 21st Jul , 2022

Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Ngollo Malenya, ameagiza kukamatwa kwa wazazi wawili Thomas Ulanda na Adelyda Nakashawa, baada ya kuwatelekeza watoto wao watatu wanaoishi Kijiji cha Gombe, huku mmoja ambaye ni wa kidato cha nne akipambana kuwahudumia wadogo zake.

Katikati ni watoto watatu waliotelekezwa na wazazi wao, kulia ni DC Ulanga, Ngollo Malenya, na kushoto ni wadau wengine

Wazazi hao waliachana, mwanamke akaolewa na mwanaume mwingine na Baba akaoa mwanamke mwingine na kuwatelekeza watoto wao kwenye kijumba ambacho muda wowote kitaanguka na kimewekewa miti kusimamisha ukuta.

Kufuatia hali hiyo DC Ngollo kwa kushirikiana na wadau wengine akachukua hatua za haraka kunusuru hali hiyo ambapo mdau John De Vries, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Faru Graphite, ameahidi kuwajengea nyumba na kuhakikisha mabinti hao wanasoma.

DC amewapongeza m ajirani wa eneo hilo waliojitolea kuwasitiri watoto hao hasa wakati wa masika na wakati wa njaa huku akiziomba asasi za kiraia zinazopambana na haki za watoto na wanawake waunge mkono hatua alizochukua.