
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP Menradi Sindano
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP Menradi Sindano amesema awali majambazi hao walivamia soko la Kijiji hicho majira ya saa 1 usiku wakiwa na silaha mbalimbali ikiwemo bunduki aina ya AK47 waliyotumia kutishia wananchi kabla ya kuanza kupora mali zao.
Aidha kamanda Menrad ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa kukishirikiana na raia wema walifanikiwa kuwafurusha majambazi hao ambapo katika majibizano ya risasi majambazi wawili wamuwawa na mmoja kutoweka kusikojulikana.
Pamoja na mafanikio hayo kamanda Menradi amewataka wakazi wa Kigoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.