
Mbunge wa Viti Maalum, mkoa wa Kagera, Neema Lugangira
Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 25, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio.
"Mimi nadhani ni kati ya watu wanaopitia ukatili wa kijinsia mtandaoni kwa kiwango kikubwa, naona siku zinavyozidi kwenda wanapunguza wenyewe, nilishawahi kupitia tukio mpaka wanangu wakaniambia kwanini natumia," amesema mbunge Neema
Aidha ameongeza kuwa, "Wanasiasa wanawake wanapitia sana ukatili wa kijinsia mtandaoni, kuliko wenzetu wanaume, unaweza uka-post hoja yako lakini mtu pale atapita anaangalia umevaaje, nywele imekaaje, hoja inahamishiwa kwenye ujinsia,".