Jumatatu , 25th Jul , 2022

Rais Samia Suluhu Hassan, amependekeza kwa ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma, kutenga eneo kubwa na bora zaidi kwa ajili ya kujenga mnara wenye hadhi ya makao makuu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 25, 2022, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma, sambamba na kushauri kwamba maadhimisho ya namna hiyo yawe na gharama nafuu.

"Kwa kuwa jiji la Dodoma linakuwa, nipendekeze kwa Waziri Mkuu ofisi yako pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma kutafuta eneo kubwa na bora zaidi ili kujenga mnara wenye hadhi ya makao makuu ya nchi kwa gharama nafuu," amesema Rais Samia