Jumatatu , 25th Jul , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora  limepiga marufuku  hatua ya walinzi wa jadi maarufu kama Sungusungu kukamata wahalifu na kuwashushia vipigo vizito ambavyo wakati mwingine vimekuwa vikiwapelekea kupoteza maisha kabla ya kufikishwa mikononi mwa Polisi

Ni wanaume kwa wanawake  wakiwa katika  hali ya utayari wakionesha madaha ya  namna walivyo jiimarisha  katika suala la ulinzi na usalama  kupitia jeshi la jadi sungusungu.

Kamanda wa  Jeshi la     Polisi Mkoa wa Tabora wakati akizungumza na  jeshi hilo la jadi amewambia  hawapaswi kutumia nguvu  zenye madhara makubwa kwa wahalifu ikiwemo kuua pindi wanapo wakamata.

Kamanda amesema suala  la ulinzi  na usalama ni jukumu  la kila mwananchi kwa mujibu wa sheria .