
Gari la basi lililopata ajali
Ajali hiyo imetokea hii leo Julai 26, 2022, wakati watoto hao wakitolewa majumbani kupelekwa shuleni na ajali hiyo imetokea baada ya breki ya gari la shule kufeli wakati likiteremka kwenye mlima katika eneo la Mjimwema.
Watoto waliojeruhiwa katika ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Mtwara ya Ligula.