
Diwani wa kata ya Buhongwa Joseph Kabadi amesema alipigiwa simu na wananchi na kuukuta mwili huo ukiwa unaelea kwenye bwawa hilo
Yusuph Msalangi ni Mwenyekuti wa mtaa wa Nyaluhama lilipotokea tukio hilo ameesema bwawa hilo limekuwa likitumika kwa huduma ya maji kwa wananchi kutokana na changamoto ya maji huku akielezea matukio mengine ya vifo yaliyotokea katika bwawa hilo.
Mwili huo tayari umetolewa ndani ya bwawa hilo lakini mpaka EATV inaondoka katika eneo la tukio bado ulikuwa haujafahamika na chanzo cha tukio hilo hakijafahamika