
Max Verstappen dereva wa kampuni ya magari ya Red Bull
Kwa ushindi huu wa Leo dereva huyo raia wa Uholanzi amefikisha alama 258 akiwa ndio kinara kwenye msimamo wa madereva na anaongoza kwa tofauti ya alama 80 dhidi ya Charles Leclerc dereva wa Ferrari aliyenafasi ya pili akiwa na alama 178.
Kwenye mbio za leo za Hangarian GP nafasi ya pili na ya tatu wameshika madera kutoka Mercedes Lewis Hamilton nafasi ya pili na nafasi ya tatu imeenda kwa George Russell. Ni mbio za 5 mfululizo Hamilton anamaliza kwenye nafasi 3 za juu msimu huu.