
Kulia ni mtoto Cellie Mwambe, na kushoto ni Cecil Mwambe
Akizungumza hii leo Agosti 24, 2022, na East Africa TV & EA Radio digital, mbunge huyo amesema kwamba, mtoto huyo baada ya kujirusha alienda upande wenye kina kidogo na kujigonga chini na kwamba alichelewa kutolewa majini ili kupelekwa hospitali.
"Hakukuwa na watu wazima karibu hivyo akanywa maji mpaka walipokuja kumuokoa ikawa 'late' walivyomfikisha hospitalini ikashindikana kumuokoa, alifia hospitali baada ya kuwa amekunywa maji mengi nadhani hata pale alipojiganga alipata jeraha kubwa," amesema Mbunge Mwambe.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa Ijumaa ya Agosti 26, 2022, jimboni Ndanda.